Popular Posts

Tuesday, February 22, 2011

TANROADS PAMOJA NA UMATI WAENDELEA NA ZOEZI MBOGA

Mmoja kati wa waelimishaji wa Mpango shirikisha wa matumizi bora ya Barabara ya Chalinze Segera Tanga ndugu Deo Mutta akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Msingi Mboga Wilaya ya Bagamoyo namna ya kuvuka Barabara kwa tahadhali.
Wadau wa Muziki hususani Twanga Pepeta je Mnamkumbuka mama huyu?

JE HUU NDIYO MAANA YA KUWA KIOO CHA JAMII?

Najaribu kutafakali na kujiuliza pale Msanii Maarufu anapoonekana kumrubuni binti mdogo na kumpa uja uzito na baadaye kuahidi kumtumza bila kumuoa, inakuwa ni kumsaidia au kumharibia maisha? Nimgependa wadau wote wajaribu kutoa mawazo na michango yao juu ya suala hili kwa kina kidogo.


Thursday, February 17, 2011

JE KUONDOKA KWA WANAMUZIKI WA TWANGA PEPETA KWENDA BENDI YA EXTRA BONGO NI KUKOMAA KWA DEMOKRASIA YA MUZIKI NCHINI?

Ni jambo lisilo pingika kuwa Bendi ya Twanga Pepeta ni mahali ambapo wasanii wengi wa TASNIA ya muziki huwa wanalilia kwenda. Jambo ambalo limenishangaza na kunistua ni kuondoka kwa Wanamuziki Saba na baadaye mmoja kuamua kurejea kwenye bendi siku mbili tu baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Bendi hiyo Kamalade Ally Choki.

Wanamuziki walioripotiwa kuondoka ni pamoja na Saulo Fargason, Rogat Hegga Catapiller, Nyamwela, Danger Boy, Otilia Boniphace, Hosea Bass na George Kanuti ambaye amerejea tena kwenye Bendi yake. Habari zinadai kuwa bado Mkurugenzi wa Extra Bongo anakusudia kuwachukuwa wanamuziki wengine ili kuimarisha Bendi yake.

Ikumbukwe kuwa bendi ya Extra Bongo ilishakuwepo kwa kipindi fulani na baadaye kuvunjika miaka michache iliyopita. Sasa najiuliza ni sababu gani zinazopelekea kwa wanamuziki hawa kuondoka kwenye bendi ya Twanga Pepeta. Je? Ni suala la Maslahi kama wanavyodai? La hasha naingiwa na wasiwasi kwakuwa wanamuziki wawili toka Bendi ya Extra Bongo ambao najua wazi kuwa uwezo wao ni Mkubwa wamerejea Twanga Pepeta, sasa kama Bendi hii haina maslahi mbona hawa wamekimbia huko kwenye maslahi. Wadau wa muziki ninaomba maoni yenu juu ya suala hili.

MABOMU YA MBAGALA NA GONGOLAMBOTO YANAFUNDISHO GANI KWA WATANZANIA?

Matukio ya milipuko ya Mabomu yaliyotokea Mbagala na Gongolamboto yanatufundisha kuwa Umakini ni muhimu sana katika maisha ya kila siku. Hakuna kitu kibaya kama dharau ambayo mwisho wa siku inapelekea watu wasiokuwa na hatia kupoteza maisha makazi na kupata vilema vya maisha. Ni vyema Watanzania tukajifunza kitu kupitia matukio haya. MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

MPANGO SHIRIKISHI WA KUELISHA JAMII BARABARA YA CHALINZE SEGERA TANGA

Wakala wa Barabara Tanzania - TANROADS kwa kushirikiana na Chama cha Malezi Bora Tanzania (UMATI) wapo kwenye zoezi la kuwaelimisha watu waishio kandokando ya barabara ya Chalinze Segera Tanga. Kwa kuanzia katika Mkoa wa Pwani Vijiji kumi na Tatu vitafaidika na mpango huu, Vijiji hivyo ni pamoja na; Bwilingu (Chalinze), Msoga, Mboga, Lunga (Lugoba), Saleni, Mazizi, Msata, Lupungwi, Mandera, Kihangaiko, Kimange, Mbwewe na Kwang'andu.

Timu ya wataalamu wa masuala ya Mazingira, Usalama barabarani, Ukimwi na Nyenzo za Kati za Usafiri wameshaanza zoezi hilo na sasa wapo kijiji cha Saleni na tayari wameshafanya zoezi hilo kwenye vijiji vya Bwilingu, Msoga, Mboga, Lunga na Saleni. Taarifa zaidi zitakuwa zinatolewa siku hadi siku.