Popular Posts

Wednesday, March 23, 2011

DEO MUTTA: AJALI YA WANAMUZIKI WA BAND YA FIVE STAR MODERN TA...

DEO MUTTA: AJALI YA WANAMUZIKI WA BAND YA FIVE STAR MODERN TA...: "MUNGU ANAJUA ATENDALO RIP WANAMUZIKI WETU WA 5STARS UKAIDI wa dereva wa basi dogo aina ya Coaster ndiyo uliosababisha vifo vya wasanii 13 w..."

AJALI YA WANAMUZIKI WA BAND YA FIVE STAR MODERN TAARAB

MUNGU ANAJUA ATENDALO RIP WANAMUZIKI WETU WA 5STARS

UKAIDI wa dereva wa basi dogo aina ya Coaster ndiyo uliosababisha vifo vya wasanii 13 wa kikundi cha taarabu cha Five Stars Modern Taarab cha Dar es Salaam. Inadaiwa kuwa dereva huyo aliyetajwa kwa jina moja la Chala alikaidi ushauri wa abiria aliomtaka apunguze mwendo, akalogonga lori la mizigo lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara kuu ya Iringa – Morogoro katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi. 

Basi hilo namba T351 BGE lililokuwa katika mwendo mkali liligonga lori aina ya Scania namba T848 APE lililokuwa na tela namba T559BDL lililokuwa limesheheni mbao na kuegeshwa katika kijiji cha Doma, wilayani Mvomero baada ya kuharibika. Katika ajali hiyo watu 12 walikufa papo hapo na mwingine aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

Marehemu alikuwa mwimbaji katika bendi hiyo, ndugu zake wamemtambua kuwa ni Haji Mzaniwa (38), Miongoni mwa waliokufa ni pamoja na Meneja wa bendi hiyo, Nassoro Madenge , mwimbaji mahiri wa taarab, Issa Kijoti na wasanii wengine mashuhuri. Kijoti ndiye aliyeimba wimbo maarufu wenye maneno Nichumu Nichumu tena, Mwaah, amekufa siku yake ya kuzaliwa, alizaliwa Machi 21, 1985. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Ibrahim Mwamakula, alisema ajali hiyo ilitokea saa 2.30 usiku. Kwa mujibu wa Kamanda huyo, dereva huyo aliligonga lori
Baada ya kuona hali hiyo dereva alibabaika, basi likayumba na kujibamiza kwenye lori hilo na paa la basi hilo kung’oka.

“Ni ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, na waliokufa wote ni waliokuwa kwenye basi dogo la wasanii wa Five Stars na kusababisha majeruhi tisa kulazwa,” alisema Mwamakula. Kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake, ambapo majeruhi ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa ni pamoja na Mwanahawa Ally (55) wa Kundi la East African Melody ambaye alikuwa mwalikwa katika safari hiyo , Susana Benedict (32), Zena Mohamed (27), Samrla Rajab (22) na Mwanahawa Hamis (36)walioko wadi namba tatu. . Kwa mujibu wa Kamanda huyo wasanii wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Ally Juma (25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis, Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa (22). 

Akihojiwa jana akiwa hospitalini alikolazwa, Mwanahawa alisema, dereva alionywa na abiria kuhusu mwendo wake wa kasi, lakini akakaidi na kuendelea na uendeshaji wake mbovu uliowasababishia ajali.“Kwa kweli dereva wa gari letu alikuwa akiendesha kwa kasi tangu tulipokuwa kukiteremka kwenye milima ya Kitonga … niliingiwa na wasiwasi juu ya mwendo wake na ndipo tulipofika karibu na Doma, tumepata ajali mbaya sana, iliyosababisha wenzetu 13 kufa na sisi kama watu tisa kupata majeraha wengine ni makubwa,” alisema Mwanahawa. Alithibitisha kuwa dereva wa gari lao alitaka kulipita lori lililoharibika, lakini ghafla kukawa na gari lingine likitoka mbele yao, “aliligonga hili lililobeba mbao na kuhama njia kwenda kujigonga usoni mwa lori lingine na kuangukia bondeni,” alisema msanii huyo mkongwe wa muziki huo.

Wakizungumza katika eneo la ajali usiku huyo, mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo, Joseph Njiwa na Nania Msemwa, ambao walikuwa na gari kubwa la mizigo wakitoka Dar es Salaam kwenda Makambako, Iringa, kwa nyakati tofauti walisema ajali hiyo ilitokea saa mbili usiku. “Ni ajali ya kutisha, tumeshuhudia basi dogo hilo likigonga lori kwa nyuma na kuhama na kwenda kugonga kichwa cha lori lingine, na watu walikatika vichwa na viungo vyao … hata sisi tuliingiwa na hofu kubwa ya kutoa msaada, lakini tulikazimika kufanya hivyo,” alisema Msemwa. Njiwa alisema, iwapo dereva wa basi dogo angekuwa na mwendo wa wastani , ajali hiyo ingeepukika kwa kusubiri lori hilo lililokuwa katika upande wake kupita na yenye kuendelea na safari hiyo. Hata hivyo alitoa lawama kwa lori lililoharibika eneo hilo kwa kushindwa kuweka alama za kuashiria kuharibika na hivyo kuepusha ajali hiyo. Baadhi ya ndugu wa marehamu waliwasili usiku wa manane siku ya tukio baada ya kuarifiwa na majeruhi na kuchukua hatua za kuchukua miili ya wasanii hao kwa ajili ya kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa mazishi. Hata hivyo miili ya marehemu hao ilihifadhiwa katika mochwari ya Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya utaratibu mwingine zaidi. Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi kutokana na vifo hivyo. “Binafsi nimeguswa na msiba huu kwa vile umetupotezea wasanii ambao walikuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza sanaa ya muziki wa taarab nchini kwetu. Hili ni pigo kubwa si kwa usanii wa taarab bali kwa Taifa letu zima la Tanzania,” alisema Rais Kikwete katika salamu zake. Aliongeza: “Nakutaka Waziri kupitia kwako ufikishe salamu zangu hizi za rambirambi kwa ndugu wa wafiwa wote. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao katika wakati huu mgumu na kuwa msiba wao ni msiba wetu sote.”

Rais Kikwete alisema anamwomba Mwenyezi Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu wote huku akiwaomba waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo mbaya kuwa na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Vilevile aliwaombea kwa Mwenyezi Mungu wote waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo mbaya wapone haraka ili waweze kurejea katika hali yao ya kawaida na kuungana tena na familia, ndugu, jamaa na marafiki zao. Waziri Nchimbi amesema, amepokea kwa mshituko mkuvwa taarifa za ajali hiyo, na kwamba ni pigo kubwa kwa tasnia ya muziki wa taarab nchini. 

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali hiyo na linaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo ya msiba huu mkubwa na wa kihistoria. “Kifo cha wasanii hawa ni pengo kubwa kwa familia na sekta ya sanaa nchini, kwani kupungukiwa na wasanii wabunifu 13 kumerudisha nyuma kimaendeleo sekta hii nchini na pengo hilo haliwezi kuzibika kwa njia yoyote iwayo,” ilisema taarifa ya Basata. Baraza limetoa Sh. 500,000 za rambirambi kwa kundi la Five Star Modern Taarab ili zigawanywe kwa wafiwa na kusaidia shughuli za msiba huo mkubwa katika tasnia ya sanaa nchini. 

Mmoja wa waratibu wa shughuli za msiba huo, Kiongozi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka amesema, wengi waliokufa alikuwa ni wasanii vijana, na kwamba, kabla ya kujiunga na bendi hiyo walikuwa katika bendi nyingine ya taarab iitwayo Jahazi Modern Taarab. Kiongozi wa Jahazi, Mzee Yusuf, amesema, vifo vya wasanii hao ni janga la taifa kwa kuwa vinawahusu hata wasiopenda muziki. “Hili janga si la Five Stars, ni letu sote Watanzania, wapenda muziki na wasiopenda muziki” amesema na kuongeza kuwa wote waliokufa aliwahi kufanya nao kazi kwa muda mrefu
Mungu awalaze mahali pema peponi marehemu wote na awasaidie waliojeruhiwa waweze kupona haraka na kuwapa nguvu ndugu,jamaa na marafiki wote katika wakati huu mgumu.Amina

ONYO: BAADHI YA PICHA NI ZA KUTISHA.TAFADHALI USIFUNGUE KUANGALIA KAMA HUNA UWEZO WA KUSTAHIMILI
 
Wanamuziki wa Bendi ya Five Star Modern Taarab
Mwanamuziki Issa Kijoto Enzi za Uhai wake
Waziri Emanuel Nchimbi akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya miili ya Marehemu kuwasili
Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka naye alikuwepo, Nyuma yake ni Said Mdoe wa Screen Masters

Mazishi ya marehemu Mussa Kijoti nyumbani kwao Mtoni

Msafara wa Askali wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati Miili ya Marehemu inawasili Temeke

Pichani ni Mwimbaji Mwanahawa Ally,alikuwemo katika ajali hiyo.Yeye alikuwemo katika msafara kama mwimbaji mwalikwa

Mashuhuda wa ajali wakihakikisha kama hakuna majeruhi au maiti iliyobakia ndani ya gari
Tochi zilitumika ili kuwatafuta watu kwa ajili ya Giza

Pichani ni mmoja wa waimbaji akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro
Pichani ni mmoja wa waimbaji akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro
Mabaki ya ya basi lililokuwa limebeba Wanamuzi wa Five Star.




Mabaki vyombo vya muziki vya Bendi hiyo
Hapa kweli katoka mtu jamani HATARI KUBWA
Mabaki ndani ya gari la Wanamuziki wa Bendi hiyo
Mabaki ya baadhi ya Viungo vya Wanamuziki wa band

Mabaki ya ya basi lililokuwa limebeba Wanamuzi wa Five Star
Mabaki ya ya basi lililokuwa limebeba Wanamuzi wa Five Star
Mabaki ya ya basi lililokuwa limebeba Wanamuzi wa Five Star
Pichani ni baadhi ya miili ya marehemu ikiwa chumba cgha maiti Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es salaam kwa mazishi.